NAFASI ZA KAZI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII 13-10-2021
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara
ya Maliasili na Utalii anakaribisha maombi ya kazi kutoka
kwa Watanzania wenye sifa na
uwezo wa kujaza nafasi Mbili (02) kama zilivyoainishwa
katika tangazo hili.
AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II - (NAFASI 1)
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki;
ii. Kutangaza Sera na Sheria za ufungaji nyuki;
iii. Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki;
iv. Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki;
v. Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki; na
vi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Msimamizi wa
kazi.
Kuajiriwa wenye Shahada katika moja ya fani zifuatazo,
Ufugaji Nyuki, Sayansi ya Elimu
ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es
Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara
TGS D.
AFISA
WANYAMAPORI DARAJA LA II- (NAFASI 1)
i. Kutekeleza kazi za ushirikishaji wadau katika uhifadhi;
ii. Kudhibiti utoaji wa leseni za biashara ya nyara na
vibali vya kukamata
wanyama hai;
iii. Kushiriki katika kusuluhisha migogoro ya matumizi ya
wanyamapori;
iv. Kudhibiti matumizi haramu ya leseni za uwindaji na
kuhakikisha kufuatwa kwa
maadili katika kutumia wanyamapori;
v. Kudhibiti matumizi haramu ya wanyamapori;
vi. Kufuatilia utekelezaji wa miongozo mbalimbali ya
uhifadhi wanyamapori;
vii. Kuhakiki viwango vya kukamata wanyama hai kwa ajili ya
biashara na ufugaji;
viii. Kufanya kazi za kuzuia ujangili;
ix. Kukusanya taarifa na takwimu za Uhifadhi;
x. Kutekeleza kazi za uhifadhi katika Mapori ya Akiba; na
xi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Msimamizi wa
kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyamapori kutoka
Chuo Kikuu
kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara
TGS D.
MASHARITI YA JUMLA
KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri
usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na
wamejipatia sifa za
kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua
zao za
maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri
wajiridhishe
ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza
(Wasifu Binafsi)
yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina
ya wadhamini
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo,
nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia
kiwango hicho na vyeti
vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika.
- Cheti cha Shahada ya Uzamili/Shahada/Diploma ya Juu/
Diploma/Cheti.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Cheti cha mafunzo ya Kompyuta
- Vyeti vya kitaaluma kutoka katika Bodi husika
vi. Vyeti vya ushiriki wa mafunzo (Testimonials), Hati za
matokeo ya mafunzo
za muda (Provisional Results), Taarifa za Matokeo (Statement
of results),
Hati za matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM
VI
RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti
vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (Tume ya Vyuo
Vikuu
Tanzania (TCU), Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) na
Baraza la Taifa
la Elimu ya Ufundi (NACTE).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma
hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za
kuingilia walioko
katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia
maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30
Novemba,2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika
watachukuliwa hatua za
kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 26, Oktoba,
2021.
Muhimu, kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwapamoja
na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/
Comments
Post a Comment