Posts

Showing posts from October, 2021

NAFASI ZA KAZI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII 13-10-2021

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi Mbili (02) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili. AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II - (NAFASI 1) MAJUKUMU YA KAZI i. Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki; ii. Kutangaza Sera na Sheria za ufungaji nyuki; iii. Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki; iv. Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki; v. Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki; na vi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Msimamizi wa kazi. Kuajiriwa wenye Shahada katika moja ya fani zifuatazo, Ufugaji Nyuki, Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali. MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D.     AFISA WANYAMAPORI DARAJA LA II- (NAFASI